Jumamosi, 28 Januari 2017

FINANCIAL TRIANGLE PRINCIPLES

                      

                         Habari za kuamka ndugu msomaji wa VIPAUMBELEKWANZA?

                            Binafsi namshukuru Mungu kwa kuniamsha salama. Leo nataka 
                             kuzungumzia uhusiano wa  FEDHA, SOKO na MIMI katika kuon

                            goza matumizi yetu ya fedha (the triangle financial principles).

                    Je unapokuwa unafanya manunuzi mahali popote nani huwa anakusukuma 
                    kununua hicho unachonunua, je ni nafsi yako au ni nguvu ya soko au nguvu 
                    ya fedha? Tathmini huu uhusiano ujue anayefanya maamuzi katika matumizi
                       yako ya fedha. Maana ukifuatilia utagundua kuwa kuna watu wakiwa na hela
                   wanaweza kununua chochote wanachokiaona hata kama kwenye bajeti hakipo.

          Na watu utawasikia wakisema pesa walizo nazo haziwatoshi. Kuna kundi lingine
        la watu wao husukumwa kufanya matumizi ya hela na FEDHA. Fedha walizo nazo
           zimetawala mioyo yao kwa hiyo mioyo yao haina nguvu kabisa juu ya fedha.
           Watu hawa akiwa na hela anaweza nunua chochote na hata kisicho na manufaa
             kwake (non-essential item). i.e. The MONEY controls them. Hata maandiko 
            matakatifu yametuonya kuwa tusiipende fedha, maana yake isitutawale.
           Lakini haimaanishi kuwa na fedha ni dhambi la hasha na wala msinielewe hivyo.
            
           Kundi la tatu hufanya matumizi yao ya fedha kwa kusukumwa na( the Me Factor)
          na mioyo yao katika kutekeleza bajei yao. Wanafanya wanachofanya pasipo kusukumwa na soko wala fedha. Watu hawa mara nyingi wana nidhamu kubwa ya pesa.
          Ushauri wangu kwako msomaji, jitahidi usiongozwe na soko wala fedha katika kufanya matumizi yako usije ukajikuta unakosa hata mtaji. Maana ukiongozwa na soko 
 ni rahisi kujikuta katika madeni yasiyo ya lazima. Si unajua kuna madeni yaliyo ya lazima 
 na yale yasiyo ya lazima. Jitathmini ujue uko kundi lipi ili usitumie fedha zako bila mpangilio.
                  Tusiwe watu wa lawama tu siku zote kumbe sisi wenyewe ndo vyanzo vya uhaba wa pesa. Mwombe Mungu katika Kristo Yesu aimarishe fikra zako ndani yako na jizoeze kutoa sadaka kwa imani na sio kwa sheria. Sadaka inaondoa akili yako kwenye kifungo cha soko au Fedha. 
                      Nawatakieni Jumapili njema na siku njema. Wako mwezeshaji katika safari hii ya mafanikio.

MAMBO UNAYOPASWA KUJUA ILI UWE MCHUMI MZURI

 Habari za mchana rafiki wa safari ya mafanikio! Poleni na shughuli za hapa na pale.
Wiki ijayo nitaanza kuzungumzia vipengele vifuatavyo:
  1. Namna ya kujitoa kwenye madeni
  2. Fedha iliyo mkononi mwako
  3. Misingi ya fedha na tabia zake
  4. Nidhamu ya pesa
  5. Jambo moja kubwa usilopaswa kusahau juu ya Pesa
  6. Uhusiano wa biashara na Fungu la kumi
  7. Heavenly account
  8. Uwekaji akiba unaotakiwa N.K.

Ijumaa, 27 Januari 2017

KIZUIZI KIKUBWA CHA MAFANIKIO YAKO HIKI HAPA

             
 Habari za kuamka ndugu zangu! Mimi nimeamka salama namshukuru Mungu kwa kutupa 
kibali tena siku ya leo..Haijalishi umeamkaje kiafya, kiuchumi n.k. jipe moyo mkuu hayo ni mapito tu..Kila jambo lina mwisho wake.
 Asubuhi hii naomba tutafakari kwa pamoja huu ujumbe. Unakijua kizuizi (obstacle) kikubwa
katika kufikia mafanikio yako kiuchumi? Vipo vizuizi vingi sana, na kila mmoja akipewa nafasi ya kujitetea nina uhakika tutapata vizuizi vingi sana. Lakini nina uhakika kama wote tutatafakari ipasavyo tutakubaliana..
        
         Kizuizi hiki ni MAAMUZI tunayofanya tupatapo pesa katika kutekeleza VIPAUMBELE VYETU, ziwe nyingi au chache..
Mwaka 2015 mimi na rafiki yangu mmoja hivi, tulipata fursa ya kikazi kwenda mkoa fulani,
tulifanya yaliyotupeleka huko kwa muda wa wiki mbili hivi. Baada ya trip hiyo tulilipwa kiasi cha Tsh.900, 000/= kila mmoja. Baada tu ya malipo hayo kila mmoja wetu alifanya MAAMUZI mara moja juu ya FEDHA hizo tulizopata. Huyu rafiki yangu alinunua zawadi nyingi sana akawapelekea wazazi na ndugu zake wengine. Baada ya muda wa miezi 2 akaniambia "my friend pesa ni mavi ya shetani". Nikamuuliza kwa nini? Akasema "huwezi amini ile hela yote imeisha na sijaifaidi". Nilimjibu hivi: Acha kulalamika hayo ndiyo MAAMUZI uliyo fanya mwenyewe, lazima uvune ulichokipanda. Naomba nikueleze jambo hili, siku zote upatapo pesa iwe ndogo au kubwa , jizoeze kutuli kwanza moyoni mwako, kisha fanya maamuzi stahili ambayo hayatakuacha na masononeko. Kumbuka hili kila siku
KILA PESA UNAYOIPATA INAWEZA KUKUTAJIRISHA AU KUKUFANYA MASIKINI ikiwa utafanya maamuzi mazuri au mabaya. 
            Rafiki yako katika safari hii ya mafanikio. Nakutakia shughuli njema!


      

UNAMJUA ADUI YAKO MKUBWA ANAYEKUZUIA KUFANIKIWA KIUCHUMI?


              Unamjua adui yako mkubwa anayekupofusha usione mahali pa kukanyaga? Adui huyo ni kulalamika...ngoja nirudie ni "kulalamika kwako" unapoona mambo hayaendi. Unafikiri ukilalamika ndo mambo yanaenda/kufanyika ipasavyo? Mahali napofanyia kazi asilimia zaidi ya 60% wanailalamikia serikali, wengine wanawalalamikia wazazi eti hawakuwasomesha, 
wengine wanajuta kuzaliwa Tanzania , wengine wanalalamikia 
course (kozi) za masomo waliyosomea. Wote hawa wanalalamika.
        
             Unategemea kweli hawa watu waone FURSA katika FIKIRA zao? Nakwambia ukweli hawataziona kamwe. Dawa ya kwanza nayokufundisha kama na wewe unalalamika, ACHA KULALAMIKA KUANZIA SASA HIVI, na utubu juu ya chambo 
hili ili Mungu akufumbue macho upya utazame mazingira KIFURSA...Haijalishi kipato ulicho nacho, usilalamike hata kidogo.. Endelea kufuatilia hii makala utajifunza mengi zaidi...
             Wako rafiki katika safari hii ya mafanikio...Amani nawatakia..