Ijumaa, 3 Machi 2017

KWA NINI UNAHITAJI MKOPO?

Habari za asubuhi rafiki yangu!
Binafsi sijambo, namshukuru Mungu.
Leo nataka tujifunze namna ya kuchukua maamuzi sahihi tunapochukua MIKOPO (LOANS) katika kufanya biashara na matumizi mengine.

Ndugu msomaji wa mtandao huu; nina uhakika unajua kuwa mwanadamu maadamu yu hai hana budi anahitaji kuwa na fedha awe mkubwa au mdogo, awe tajiri au masikini, wote tunahitaji fedha. Huu ndio ukweli wa mambo.
Na katika uhitaji huu, uchumi wa dunia umekuwa ukijifunza na kufanya tafiti nyingi juu ya kuhakikisha kila mtu ili aweze kufanya biashara lazima ahitaji pesa au hela au fedha. Na kwa sababu hiyo, benki nyingi na taasisi mbalimbali duniani zimeanzisha mfumo wa kukopesha na kurudisha faida (riba) kwa aliyekukopesha fedha hizo (loan).

Ndugu rafiki yangu, shida imekuja pale wakopaji wanapojidanganya wakidhani mkopo ni msaada au huduma ya kusaidia wasiojiweza. Namaanisha nini?
Namaanisha kuwa unapokopeshwa fedha ujue aliyekukopa, anahitaji na RIBA katika fedha hiyo, upate hasara au upate faida lazima umrudishie fedha zake pamoja na RIBA. Na si kosa kumpatia RIBA mkopeshaji kwani anafanya biashara. 
Riba ni faida utakayomzalishia kwa kipindi maalumu mnachokubaliana kimkataba.
Nachotaka ufahamu ni hiki, aliyekukopa anafanya biashara na wewe, na ukiwa mzalishaji bora unakuwa mwaminifu kwa aliyekukopa.
Zingatia jambo hili: MKOPO ni BIASHARA.
Kwa kuwa siku hizi kumekuwa na ukosefu wa mitaji, taasisi mbalimbali za kifedha zilizo rasmi na zisizo rasmi zimeanzisha huduma za mikopo tena kwa urahisi zaidi, na kadri siku zinavyoendelea, huduma hii ya mikopo inazidi kupamba moto.
Na wahitaji kwa kutokujua hili, wamechangamkia FURSA hizi bila kujiuliza maswali, na hali zao za maisha wengine zimeyumba jumla. Sisemi kwa kukuogopesha, nasema ili ufanye maamuzi mazuri katika masuala ya mikopo.

Natamani nikushauri jambo moja kubwa! Siku zote unapochukua mkopo jiulize maswali yafuatayo:
1.Mkopo huu unatolewa na taasisi ipi?
Si watu wengi sana wanaotafuta mikopo wanajiuliza swali hili, wao wanachotaka ni hela tu, mengine baadaye! Kuwa mwangalifu juu ya hili. Unapotaka kukopa, fuatilia kutaka kujua hiyo taasisi ikoje. Ndiyo maana wengine wameumizwa jumla na wameporomoka kimaisha kwa sababu ya mahali walipochukua mikopo. Nakumbuka mwaka fulani, kuna taasisi walianzisha mfumo fulani, ukitaka mkopo, unatoa hela za kwako kwanza, wao wanakuambia kuwa, inabidi uwekeze kwanza kwao kisha baada ya muda wao watakukopesha fedha za kukutosha. Na kwa kuwa unakuwa na kiu ya fedha, unajikuta umetoa fedha zako. Ndugu msomaji, na mwaka huo watu wengi walitoa fedha zao na mpaka leo, hiyo taasisi ilikopotelea hakujulikani. 
Kumbuka kuwa, kuna uhusiano wa karibu kati ya fedha na hali ya kiroho ilikotoka fedha hiyo. Na hiyo roho itafuatilia hizo fedha. Ndiyo maana kuna sehemu ukikopa fedha huzifanyii chochote hata kama umejiandaa kufanya kitu fulani. Ukishazipata tu, akili inafanya kinyume, baada ya fedha kuisha ndipo unashtuka. Ikiwezekana unakopa tena na tena, mwisho wake, unaishia pabaya.
muhimu: Fanya uchunguzi wa kina wa mahali unataka kukopa fedha.

2. Unajua RIBA ya mkopo unaotaka kuchukua?
Ni muhimu na ni lazima uulize wahusika juu ya RIBA zao, na wanakokotoaje hizo riba. Waulize hizo riba ni kwa mwaka au kwa mwezi? Waulize usiwaogope, maana kuna wengine wakifika sehemu hizo utadhani wao ni malaika, waulize vizuri, ukiridhika sawa, usiporidhika achana nao, hiyo ni biashara sio huduma. Kwa mfano, unaweza ukaambiwa riba ni 1.6% , halafu wewe huulizi unajua riba nafuu. Au unafikiri nakutania? Wako watu wengi wamechukua mikopo bila kujua utaratibu wa riba.
muhimu: fahamu kwa undani utaratibu wa riba zao.

3. Je, naruhusiwa kufuta mkopo nje na muda tuliopatana?
Watu wengi hawaulizi swali hili muhimu sana, wao kwao kinachotafutwa ni fedha. Ndugu msomaji, waulize hivi: Naweza kuja kurudisha au kulipa fedha zenu hata kama ni kabala ya muda wa kimkataba? Waulize tena hivi: Mtu anapokuja kufuta mkopo wake, mnatoa riba au hamtoi? Na unapojibiwa waombe vipeperushi au maandiko yanayodhihirisha hayo. Usipende kuambiwaambiwa kwa mdomo tu. Omba kupewa nyaraka.
Lakini pia unaweza ukawauliza: Je, ikatokea nikafa, mkopo wangu utafutwa au waliobaki watawajibika nao? Omba kufafanuliwa vizuri. Kufa kupo maadamu unaishi chini ya jua.
Swali la mwisho, waulize hivi: Ikatokea nimekwama kifedha, naweza kusimamishiwa mkopo kwa muda fulani? Waulize wala usiogope!

4. Jiulize hili swali mwenyewe, "kwa nini nataka kuchukua mkopo?
Ndugu msomaji ni muhimu ujue jibu la swali hili, kwani mkopo ni fedha ya mtu amekupa uizalishe upate faida na mgawane hiyo faida. Ndiyo maana ni muhimu ujue kuwa mkopo ili uweze kumpatia faida yake mkopeshaji na wewe upate faida yako, huna budi kuizalisha. Kuna msingi mmoja wa fedha nao ni huu:Fedha huwakimbia wasiojua kuizalisha.
Usichukue mkopo kufanyia mambo ya ovyo hovyo wakati huna hata kitega uchumi kingine!
Wapo watu wanashangaza mno, wao ilimradi fedha zipo yeye atazichukua tu.

ushauri wangu kwako, usianze kuchukua mkopo mkubwa kwa mara ya kwanza, anza na kidogo ili ujue uwezo wako. Mkopo ni sawa na bunduki ya kuwindia wanyama, ukiitumia vizuri, unampata mnyama huyo, ukiitumia vibaya, unakugharimu wewe mwenyewe.

Nawatakia Jumamosi njema na baraka tele!
 

TAFUTA JIBU LA SWALI HILI MOJA TU

POLENI WOTE KWA MAJUKUMU!
Mchana huu naomba ujiulize hili swali moja tu
Nifanye nini ili nitoke kwenye hii hatua ya maisha?

Alhamisi, 2 Machi 2017

EMLOYABILITY SKILLS




MAFANIKIO NI KUWA NA VIPAUMBELE BORA

Email Address







Good evening my dear friends!
It's my hope that you are all fine.
Employability skills  are skills you need for a job.
For many people today, a career for life is no longer an option. Most people will hold jobs with a variety of employers and move across different employment sectors through their their working life.

         We all need to be flexible in our working working patterns and be prepared to change jobs and/ or sectors if we believe there are better opportunities elsewhere.

In order to be flexible we need a set of "transferable skills"- Skills that are not specific to one particular career path but are generic across all employment sectors.

The Job Skills Employers are Looking For
Employers are often looking for skills that go beyond qualifications and experience.
While your education and experience may make you eligible to apply for a job, to be successful in the role you will need to exhibit a mix of skills: "employability skills". 
This means that, the specialist, technical skills associated with different roles may be less important than the "soft skills" that can be transfered between different jobs and different sectors.
For many employers, getting the right people means identifying people with the right skills and qualities to fulfil the role and contribute to the organisation's success. Candidates may have the qualifications and "hard skills" needed to be able to manage the job role but, without a well-honed set of "soft skills", employers are less inclined to hire.

What are employability skills?
Those are skills necessary for getting, keeping and being successful in a job. They are the skills and attitudes that enable employyees to get along with their colleagues, to make critical decisions, solve problems, develop respect and ultimately become strong ambassadors for the organization.
Employment or "soft skills" are the foundation of your career building blocks and they are frequently referenced in the media as lacking in school-leavers, graduates and those already in employment (in-service).
Organisations spend a lot of money and time training staff, not in job specific areas but in general and basic skills.
NOTE: In times of high unemployment, employers have more choice of applicants and will favor those with well-rounded employability skills.
Keep in mind:
Different roles require different skill sets and abilities.
Here at VIPAUMBELEKWANZA there will forthcome a series of skills you need to help you get a job. The series are:
1. Writing a CV
2. Applying for a Job
3. Writing a covering Letter
4. Writing an effective Linked in profile
5. Interview Skills.
May you be blessed, yours author Faustin Mahende. 

Jumatano, 1 Machi 2017

JIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA ULIYOFANYA

Habari za Alhamisi ndugu msomaji wa VIPAUMBELA KWANZA! 
Natumaini unaendelea vizuri katika harakati za kupambana na maisha ili uweze kufanikiwa. Ndugu msomaji wa makala zangu, kuna kitu watu wengi wamesahau kukifanya na kinawagharimu mno. Si mara nyingi watu huwa tunajitathmini kwa nini tunakwama kila siku katika kufanikisha ndoto (vision) zetu tulizonazo.
Umewahi kujiuliza kwa nini unakwama kila wakati? 
Umewahi kukaa chini angalau muda wa hata nusu saa ili utafakari kwa nini huvuki mahali ulipo kimaisha? Wengi tukikwama huwa tunakimbilia kuwalaumu wengine, hutaona tukijilaumu na kujitathmini sisi wenyewe kwanza; na hii imetufilisi fikra zetu na mitazamo ya kimaisha tuliyo nayo (mindset).
Ulishawahi kujiuliza haya maswali? Nadhani umewahi kujiuliza. Na kama hujajiuliza leo nakushauri kaa chini ujiulize hayo maswali.
Laiti watu wengi tungekuwa na tabia ya kujifunza kutokana na makosa tunayofanya tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
Leo nataka nikupe ushuhuda wa kwangu binafsi ulionisaidia nikaanza kuvuka baadhi ya maeneo, si kwamba nimekwisha kufika, bado napambana kama wewe, ndio maana nakushirikisha ili tupambane wote kuelekea kwenye maendele na mafanikio ya maisha yetu. Unajua dunia hii ina FALSAFA nyingi sana, nyingine zinatusaidia nyingine hazitusaidii. Ni uamuzi wako ufuate "phillosophy" ipi katika maisha yako kwa kuwa maisha ni uchaguzi.

ushuhuda

Mwaka 2013 ni mwaka nimeanza kazi katika taasisi fulani hapa nchini. Nimeanza kazi hiyo pamoja na marafiki zangu kama tano (5) hivi. Nilipoanza kazi nilikuwa na malengo mengi sana na nilijua ndo nimefanikiwa kimaisha jumla. 
Maisha yaliendelea, na baada ya muda nilianza kupigiwa simu za ndugu na marafiki wakihitaji msaada wa kipesa, na mimi sikuona shaka kuwapa wakati NAJIONA kuwa fedha ninazo japo hazikuwa nyingi. Na ndugu hawa baada ya kuona wakiomba msaada kwangu hawanyimwi waliamua kunitegemea jumla bila ya mimi kujua. Baada ya mwaka mmoja na miezi kadhaa, nilianza kuingia kwenye madeni ya hapa na pale. Kilichonifanya nikajikuta kwenye madeni ni huruma zangu za kuwaokoa ndugu zangu waliokuwa wakihitaji msaada kwangu kifedha.
Maisha yalizidi kuwa magumu hata ikafika mahali nikaaanza kukata tamaa na ndoto zangu. Wakati huo nilikuwa na mchumba au rafiki wa kike niliyekuwa nimemuahidi kumuo siku si nyingi. Ghafla, ugomvi ulianza baina yangu na yeye, hii ilitokana na yeye kuona kuwa nampa ahadi hewa, na hii ni KWA SABABU SIKUMWAMBIA UKWELI KUHUSU hali niliyokuwa nayo. 
Siku moja huyo mchumba wangu alinipigia simu usiku. akaniuliza hivi: Faustine! do you really need me to be your wife? Nilimjibu , yes my dear, I do!
Ndipo aliponiuliza hivi, mbona nikikuomba hela hata elfu 10 unaniambia subiri mwisho wa mwezi? Aliongeza tena akasema, kwani kuna shida gani, ni kweli hela huna au una binti mwingine?
 Aliendelea kunilaumu sana, na wakati huo nilikuwa napigiwa simu nyumbani kwa kila tatizo lililojitokeza hata kama lilikuwa ndani ya uwezo wao. Madeni yaliendelea kunitesa nikafika mahali hta kukopa siwezi tena. Ndipo nilipoona kuwa maisha yamenishinda, japo kwa nje niliokena ninazo pesa.
Baada ya miaka 2na miezi hivi, nilikuwa hata siwezi kumudu hata kula chakula cha kushiba, nikaona sasa naelekea kufa.
Tarehe 25 ya mwezi Disemba 2015 nikiwa nasherehekea "KRISMASI" lilikuja swali moyoni mwangu, nalo lilikuwa hivi: Nitaishi maisha haya mpaka lini na huku nina AJIRA? Nikajiuliza tena, " kwa nini nisiwashirikishe wazazi wangu, na watu wa karibu kwangu juu ya hali niliyo nayo? 
Nikaamua kuwashirikisha wazazi wangu kuhusu madeni na hali niliyonayo. Nilimshirikisha pia mchumba wangu hali niliyokuwa nayo japo kwa aibu.
Wazazi wakaniambia hivi, unajua kwa nini umekwama kimaisha? Nikajibu ndiyo! Baba akaniuliza, ni nini? Nikamwambia "nina wategemezi wengi". Baba akasema "hapana". Tatizo ni wewe mwenyewe!
Alivyosema hiyo sentensi nilifikiria sana kwa nini amesema hivyo.
Ghafla nikagundua jambo lifuatalo ambalo lilibadilisha maisha yangu.
1. Niligundua kuwa nilidhani kwa kuwa ninapata pesa kila mwezi, basi nitafanikiwa.
2. Niligundua kuwa huwa sijifikirii KWANZA kabla ya kuwafikiria wengine.
3. Niligundua kuwa kila hela ndogo ninayoipata ni ya muhimu kwangu.
4. Nilifahamu kuwa, nilitakiwa nijikwamue kwanza mimi ndipo nianze kuwasaidia ndugu zangu.
5. Niligundua kuwa hata fungu la kumi si mtoaji kabisa.

UAMUZI NILIOCHUKUA.
1. Niliamua kuomba toba kwa Mungu juu ya matumizi yangu ya fedha.
2. Nilitengeneza mfumo wa kifedha wa "kuweka akiba kila mwezi " KABLA ya kupanga matumizi ya pesa.
3. Nilianza kuweka vipaumbele katika maisha yangu na kuvitendea kazi.
4. Nilianza kuwekeza pesa nyingine.
5. Nilianza kuishi uhalisia wa maisha yangu.
6.Nilianzisha chanzo kingine cha kipato nje na AJIRA, na hapa ndipo nilipoanza kufurahia maisha kwa kiasi fulani.
Ndugu msomaji, naomba nikushauri mambo yafuatayo:
1. Usiishi jinsi usivyo ili kuwafurahisha wanaokutazama, maana mafanikio yako, yako mikononi mwako.

2.Jizoeze kuweka akiba kwa kila fedha unayopata hata kama ni ndogo.

3 .Usianze kuwabeba wategemezi ulionao wakati bado na wewe umenaswa. Waeleze ukweli kuwa bado kuna mambo unayaweka sawa. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu japo ukweli haupendwi na wengi.

4. Epuka madeni, na kama unayo yalipe kwanza hata kidogo kidogo. Hutaweza kufanikiwa na kuwa huru wakati bado ni mdaiwa. LIPA DENI ULIZO NAZO, waeleze ukweli wanaokudai kuwa utaanza kuwalipa, usiwakimbie kawaeleze ukweli wa maisha yako, nao ni binadamu, watakupa utaratibu wa jinsi utakavyowalipa. DAWA YA DENI NI KULILIPA si zaidi ya hapo.

5. ANZISHA BIASHARA AU CHANZO CHA KIPATO kingine.

6. Amua kuwa utabadilika katika maisha yako, na hapo ndipo utakapoweza kuona mafanikio yako.


Mungu awabariki, wako MASTER WA VIPAUMBELE KWANZA.