Ijumaa, 24 Machi 2017

ACHA TABIA YA KUAHIRISHA MAMBO


Habari za weekend ndugu msomaji
Natumaini unaendelea vizuri na harakati za maisha na mafanikio.
Kuna jambo fupi natamani nilizungumze siku ya leo, nalo ni hili.
Kuna kundi la watu, wao maisha yao yamejaa kuahirishwa ahirishwa. Naamini umewahi kuwasikia mara nyingi. Mtu anakuja kwako, kuomba ushauri wa kufanya ili ajinasue mahali alipokwama, yeye, anakuahidi kuwa atalifanyia kazi, mwisho wa siku, anaishia kusema, unajua, sijajipanga vizuri, anakuambia mwezi ujao lazima atafanya, mwezi ukifika, hafanyi, anaahirisha tena. Ukimuuliza vipi, anakuambia, unajua mdogo wangu, wazazi wangu, n.k.

Ni kweli unachosema, lakini je, utaendelea kuahirisha mpaka lini? Hujui muda hauahirishwi, au unadhani ukiahirisha, muda unakusubiri? Hasa kwa suala la fedha, muda ni wa muhimu sana kuliko hata fedha zenyewe.
Nakuomba ujitahidi, ubadilike, uanze kuchukua hatua zinazotakiwa. 
Nikutakie mafanikio mema na afya tele


JIUNGE NA MTANDAO HUU ILI UJIFUNZE ZAIDI









0 maoni:

Chapisha Maoni