Jumapili, 5 Februari 2017
Habari za asubuhi ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA! Natumaini
umeamka salama kabisa. Sifa zirudi kwa Mungu wetu aishiye milele.
Asubuhi hii nina swali natamani nikuulize ambalo wengi wetu tunalidharau.
Swali lenyewe ni:Je, una malengo ya muda mrefu?
Watu wengi kwa kukosa elimu ya kutosha juu ya nidhamu ya
fedha, tunafikiri kwa kuwa tuna nguvu na afya na tunaingiza fedha
kila iitwapo leo, tunadhani mafanikio mazuri hayako mbali. Ni kweli
ni dhana inayoonekana kuwa sawa, lakini mwisho wa siku hutuweka
kweupe kama tuliwekeza kwa muda mrefu au La!
Unaweza kuwekeza maeneo mengi kama vile majengo, ardhi n.k.
Asubuhi hii naomba tutizame eneo la FEDHA. Ni kweli ninajua
idadi kubwa ya watu hujiwekea malengo makubwa ya muda mfupi
na ya muda mrefu. Lakini cha kushangaza ni kuona watu hao hao
mwisho wa siku hawana kitu. Kinachowakwamisha ni Utekelezaji tu.
Malengo ya muda mrefu ni yale ambayo ni zaidi ya miaka 2 na kuen
delea.
Ndugu msomaji, nakushauri kama huna malengo ya muda mrefu
anza sasa. Kwa mfano, miaka mitano (5) ijayo unatarajia kupata
kitu gani cha ziada kifedha? Sizungumzii kukua kwa biashara yako
nazungumzia "investing your money to earn for you". Weka pesa
sehemu au katika taasisi za kifedha zinazotoa na riba. Haijalishi
unapata fedha kiasi gani "wekeza fedha zako" katika taasisi husika
, mfano masuala ya hisa (soko la hisa), fanya utafiti ni kampuni gani
unaweza kuwekeza fedha zako ili zikuzalishie faida huku wewe
ukiendelea na mambo mengine.
Ngoja nikupe mfano: Kuna rafiki yangu mmoja aliweza kuwekeza
sh.50, 000 kila mwezi kwa miaka 5, akaja kuvuna sh.5, 000, 000.
Miaka 5 si mingi kama unavyofikiria. Kama uongo, nitafute mwaka
2021 uniambie ulichofanya cha maana zaidi. Mimi huwa naita uwe
kezaji wa jinsi hii "The magic of Compounding". Invest your money.
Fikiria ukiweza kuwekeza tsh.150, 000 kila mwezi kwa miaka mitano
unaweza kupata Tsh.16, 000, 000. Njoo unione baada ya miaka 5
uniambie ulichofanya. Ushauri wangu kwako, anza sasa "kuwekeza
pesa zako hata kama ni kidogo.
Kuna mtaalamu wa masuala ya uwekezaji aitwaye "DAVE RAMSEY"
anasema hivi "I cannot afford not to Invest my money".
Nikutakie siku njema!
0 maoni:
Chapisha Maoni