Jumapili, 19 Februari 2017

JE! UMESHINDWA KUTOKA KWENYE MADENI?

Ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA habari za kuamka? 
Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama kabisa japo changamoto kwa mwanadamu 
hazikwepeki awapo chini ya jua.
 Muhimu ni kujipa moyo kwani aliyekuumba yuko pamoja na wewe kila hatua. ya maisha yako.
        Ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikikwamisha wafanya biashara na wajasiriamali ni MADENI YASIYOKOMA. Ni kweli kuwa na deni sio kitu cha kushangaza sana lakini kuwa na deni lisilo la lazima ni jambo la kushangaza.
  Ukweli ni kuwa MADENI (DEPTS) yana athari sana kwa mdaiwa hasa anaposhindwa kuyalipa.
Hivi ulishawahi kudaiwa? Kama umewahi au bado unadaiwa ni muda mwafaka wa kukataa kuingia kwenye madeni yasiyo ya lazima. Wengi huwa wananiambia kuwa haiwezekani kuishi bila deni, ukifikiri jambo hili kishabiki utadhani falsafa hii ni kweli. Lakini nakiri kuwa inawezekana kutoingia kwenye madeni yasiyo lazima kama utaamua kutoka katika kifungo hicho.

Naomba tujibu swali hili kila mmoja akijitathmini: Je! ni kwa nini kila siku najikuta katika madeni?
Nitajibu swali hili kijumla (in general) kwa kuwa kila mmoja wetu anazo sababu za kwake..
Nakiri wazi kuwa zipo sababu nyingi mno zinazotufanya kujikuta katika vifungo vya madeni (FINANCIAL BONDAGE) sugu. Baaadhi ya sababu hizo ni hzi zifuatazo:
  • KUTOJIWEKEA AKIBA YA KUTOSHA
  • KUISHI MAISHA YA KUIGA
  • KUWA NA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO
  • KUTOZINGATIA MATUMIZI YA BAJETI 
  • KUWA NA WATEGEMEZI WENGI KIFEDHA
  • KUCHUKUA MIKOPO BILA MAANDALIZI
Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazotunyima uhuru wa kifedha (FINANCIAL FREEDOM).
Hakuna kitu kinanitesa kama DENI katika maisha haya. Deni ni adui wa fikra na hutuweka utumwani kwa yule au wale wanaotudai. Hivyo hatuna budi kuwa waangalifu katika matumizi ya fedha tunazopata kila siku. 
Endelea kufuatilia makala nazoandika ili upate kujifunza mambo mengi juu ya uchumi na jinsi unavyoweza kufanikiwa. Kila jambo linaanza na maamuzi. Hatuwezi kufikia UHURU WA KIFEDHA mpaka tuwe huru na madeni yaani tusiwiwe na watu. Kibaya zaidi ukiwiwa na mtu asiye na hekima utajuta. Hivyo nitakueleza njia zilizonisaidia kutoka kwenye madeni.
Karibu tuendelee kujifunza pamoja mambo mbalimbali yanayohusu maisha na mafanikio.
Wako master wa VIPAUMBELE KWANZA. Kila heri rafiki. 

0 maoni:

Chapisha Maoni