Jumamosi, 25 Februari 2017

KWA NINI HUNA BIASHARA?

Habari za usiku ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA.
Naomba tushirikiane kujibu hili swali. Nalo ni:
"Kwa nini sina biashara yoyote? Ndugu msomaji huwa nashangaa kila wakati watu wanapokuwa wanalalamika eti wameshindwa kufanya biashara. Unajiuliza kwa nini, unakosa majibu. Kuna rafiki yangu alikuja nyumbani napoishi tulipokuwa tunazungumza, aliniuliza swali lifuatalo ambalo naamini huenda na wewe linakusumbua. Swali nililoulizwa liko hivi:
"Ni biashara gani inayolipa zaidi"? Je, ungekuwa ni wewe umeuliza ungemjibuje?
Nilielewa ghafla kuwa huyu ndugu anafikiri kuwa ili ufanikiwe kuna biashara fulani unayotakiwa kufanya. Niliendelea kuzungumza naye mambo kadhaa yahusuyo maisha.

Kwa nini kila siku hili swali huulizwa? why?
Umefika wakati wa sisi kwa sisi kuelezana ukweli..
Ndugu msomaji wa hii makala, kiukweli hakuna BIASHARA nzuri kuliko zote, kwa sababu biashara ili ifanikiwe inategemea mambo mengi kama vile
  • Eneo biashara ilipo
  • Usimamizi wa biashara
  • Mtaji wa biasha
  • Uhitajiwa wa biashara.
Yapo mambo mengi sana yanayochangia biashara kukua na kufanikiwa. Unaweza ukaanza biashara ya fedha nyingi na bado usifanikiwe kama ulivyotarajia.
Hebu tujibu swali hili linaloulizwa kila siku:
KILA BIASHARA INALIPA NA KILA BIASHARA INAWEZA ISILIPE
Watu wanaouliza hili swali tatizo lao ni hofu ya kufilisika, na wengine hawana mitaji ya kuanzisha biashara. Wengi ni waoga kuanzisha biashara. Hasa wale walioajiriwa, na hii ni kutokana na elimu dunia ilivyowazoesha kulipwa, ni waoga kuthubutu. Ndugu msomaji, mafanikio yako mikononi mwako, ukiona unaogopa kuthubutu, ikiwezekana, mwombe Mungu akusaidie. 

La pili ni kutokuwa na mitaji.
Huwa siamini kuwa watu hawana MITAJI ya kuanzisha biashara. Kama ni kweli hawana, yafuatayo hujitokeza, nayo ni: 
1.Wanataka kuanza na biashara kubwa kubwa, kitu ambacho kinawachukua muda mrefu sana.
2. Au hawako serious na biashara. Kwa sababu mtu mwenye kipato cha sh.5000 kwa siku hawezi kusema hana mtaji, ni kutokuwa na matumizi mazuri ya fedha anazopata. Niliwahi kushuhudia, mtu akianza biashara kwa sh.15000 tu. Huwezi amini lakini nilishuhudia. Shida ni fikra zetu, tunataka tuwe mamilionea ndani ya siku 14, haiwezekani ndugu yangu. Anza na kidogo, uwe na uhakika utafika unakotaka kwenda.

Ukiona mtaji hakuna, kusanya nguvu na wenzako mfanye biashara kwa pamoja. Muhimu mnaoshirikiana nao wawe waaminifu na uwe mwangalifu sana. Maana biashara ya kikundi si mara nyingi mwisho wao ni mzuri. Lakini wapo wanaofikia malengo yao..

Tatu unaweza ukakopa ikiwezekana, lakini usiwe mwepesi sana kuchukua mikopo ilimradi inapatikana. Kama huna uhakika na unachotaka kuufanyia huo mkopo, usichukue maana utakugharimu.

Tukijaliwa, nitakuja kuelezea vitu vya kuzingatia unapochukua MKOPO, na maswali unayopaswa kujiuliza kabla hujachukua MKOPO.
Nikutakie usiku mwema! 
   

0 maoni:

Chapisha Maoni