Jumapili, 19 Februari 2017

MUNGU NDIYE MWANZILISHI WA NDOA

Mpendwa msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA
Bwana Yesu asifiwe! Tumsifu Yesu Kristo!
Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama kabisa, ni jambo la kumshukuru Mungu wetu katika Kristo Yesu! Ni neema na rehema tumepewa, si kwamba tunastahili, la hasha!
Ndugu msomaji wa makala hii, ningekushauri kabla ya kusoma ujumbe huu uombe uongozi wa Roho Mtakatifu ili uweze kupata kilichomo ndani yake. Tukumbuke kuwa hakuna anayejua kila kitu katika maandiko matakatifu (BIBLIA) bali tunapewa kwa sehemu (1 Wakor 13:9) "Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu).
Ndugu msomaji katika vitu ambavyo kwa kasi vinazidi kupoteza "kusudi la kuumbwa kwake ni MISINGI YA NDOA KIBIBLIA, na hii hutokana na hila za yule adui yetu Shetani anazoingiza katika ndoa kwa njia nyingi sana. Anaingiza misingi na mtazamo wa kwake wa giza kupitia elimu, mila na desturi za watu na mpaka yapo baadhi ya madhehebu yameanza kupotosha misingi ya ndoa kibiblia.
 Ikiwa kweli tunataka kuponya ndoa zetu ipasavyo, hatuna budi kuifahamu kweli ya neno la Mungu katika eneo la ndoa na kuitii na si vinginevyo (Yohana 8:32) "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru, ukisoma ule mstari wa 36 unaongeza hivi: Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli. Haleluya!
Ndiyo maana Biblia inasema " Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa" (Hosea 4:6b) 
 Ukisoma vizuri huo mstari maandiko hayasemi watu wa dunia hii, bali watu wa Mungu (waliookoka ndio wanaoangamizwa), wanaangamizwa kwa sababu gani? Hawaangamizwi kwa kuwa wana dhambi, hapana! Wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA ya neno la Mungu. Si kwamba hawaombi, wanaomba! Si kwamba hawahudhurii ibada za Jumapili au Jumamosi hapana! Neno la Mungu linasema, wamekosa maarifa yatokanayo na neno lake (Mungu). Fahamu hili: Tukijua sana; tunaweza sana. 

Ndugu mpendwa msomaji, turudi kwenye somo letu.
Naamini wote tunafahamu kuwa kila kilicho hai na kisicho hai vimeumbwa na Mungu, kama huamini, Mungu akusaidie na akutie nuru macho yako ya ndani uone sawasawa. Kwa sababu hiyo, hata NDOA imeanzishwa na Mungu kwa kusudi fulani la Ufalme wake. Katika makala hii sitazungumzia kusudi la ndoa, bali nitazungumzia MTAZAMO tunaopaswa kuwa nao juu ya NDOA kibiblia. Ukisoma (Mwanzo 2:24), maandiko yanasema hivi: " Kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake (wazazi) naye (mwanaume) ataambatana na mkewe, nao watakuwa MWILI MMOJA).Bwana Yesu asifiwe!
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili (mwanaume na mwanamke) na kuishi pamoja kama mume na mke. Hili neno nao watakuwa mwili mmoja huwa linanipa maswali mengi sana!
Kwa nini najiuliza hivi? kwa sababu wakioana bado utaona miili miwili, si ndiyo mpendwa msomaji? Lakini wakati natafakari jambo hili, liliingia wazo ndani yangu hivi:
Kwani Biblia inaposema, "Mungu ni mmoja inamaanisha nini? Mungu ni mmoja lakini katika nafsi tatu (Holy Trinity). Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Yesu alisema, "Mimi ni ndani ya baba na Baba yu ndani yangu. Lakini pia ukisoma (Waefeso 5:31-33) utakuta uhusiano wa mke na mume umefananishwa na uhusiano wa kanisa na Kristo Yesu. Yesu Kristo apewe sifa! Biblia inasema na "na hao wawili watakuwa mwili mmoja), kumbe nilifahamu ghafla moyoni mwangu kuwa, moyo wako na moyo wa mke wako vimeambatana, hivyo huwezi kutenganisha moyo wa mke na moyo wa mume. Biblia inaposema tuwe ndani ya Kristo na Kristo awe ndani yetu, haimaanishi tuingie na mwili wa nyama, hapana bali mioyo yetu iko kwake, HALELUYA!
Pointi ya kwanza nayotaka uifahamu ni hii" ILI NDOA IWE HAI LAZIMA MOYO WA MKE NA MUME VIAMBATANE. Na ili viambatane, inabidi mwanamke afanye jambo hili;
AWASAHAU WATU WA NYUMBANI KWAKE , YAANI HUKO KWA WAZAZI WAKE. Kwa lugha nyingine nafasi waliyokuwa nayo watu wa nyumbani kwao, aipe mume ili sasa waambatane.i.e. Kipaumbele cha mume kiwe cha kwanza baada ya Yesu moyoni mwake. Hebu soma (Zaburi 45:10-11). "Sikia binti utazame utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme (mume) atautamani uzuri wako, maana ndiye akupaye bwana wako naye umsujudie. Praise the LORD JESUS!

point ya pili: Mke na mume wanapaswa kuwa na sura ya Mungu ndani yao.
Biblia inasema, "Mwanzo 1:26", Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa sura yetu....mstari wa 27, ...'Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba....
Ukisoma maandiko vizuri utafahamu kuwa, Mungu ni Roho (Yohana 4:24), hivyo hazungungumzii sura ya kimwili, bali sura ya rohoni. Ukiwa na Yesu, una sura ya Mungu kwa kuwa Yesu ni sura ya Mungu. Hivyo, ukiwa na Yesu, vipaumbele vyako vyote vinatanguliza kwanza Ufalme wa Mungu. Na shetani anajua kuwa ukipoteza mtazamo wa kimungu juu ya ndoa moyoni mwako (in your soul), umepoteza sura ya Mungu ndani yako, na hivyo ndoa inaanza kupoteza mwelekeo, na kinachofuata ni kifo cha kiroho (mauti), yaani kutengwa na uwepo wa Mungu. Hivyo ukiwa na sura ya Mungu unakuwa na uwepo wa Mungu, Yesu anakuongoza kwa njia ya Roho Mtakatifu namna ya kuendesha ndoa yako na mambo mengine.

Pointi ya tatu: Hekima ya kujenga nyumba au ndoa amepewa mwanamke na si mwanaume!
Simaanishi kuwa, mwanaume hana umuhimu katika ndoa yake la hasha! Biblia isingesema, mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo Kichwa cha kanisa! Nazungumzia nafasi ya mwanamke kwa mumewe. Soma Mithali 14:1, "Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake....tukumbuke kuwa, Mwanzo 1:26-28, Mwanamke na mwanaume wameumbwa kwa sura ya Mungu, hivyo mke mwenye sura ya Mungu ana hekima ya kuijenga ndoa yake, sura ya Mungu ikipotea ndani yake, mauti inatawala ndoa, yaani wanatengwa na uso wa Mungu na wanaanza kwenda bila utaratibu wa Kimungu, na mwisho wao ni shetani kuwaangamiza (Hosea 4:6a). Mwanamke amepewa nafasi nyingi juu ya ndoa yake kibiblia. Amepewa nafasi kama vile
  1.     Mjenzi
  2. Mleta kibali kwa mumewe
  3. Mshauri
      4.Msaidizi 
Zipo nafasi nyingi sana alizopewa mke; tutaziangalia katika somo litakalofuata kwa undani zaidi.
Ndugu msomaji, napenda nikuambie jambo zito, kama hatutamgeukia Bwana Yesu na kumkaribisha katika ndoa zetu, hakika hatutaona ushindi. Lakini pia ni muhimu tuifahamu kweli ya neno lake juu ya kuwepon kwa ndoa ndipo tutakuwa huru kwelikweli. Inashangaza siku hizi kuona watu wakipewa chumvi ya kutembea nayo ili ilinde ndoa zao. Sikatai inaweza ikatokea Mungu akatumia chumvi, lakini sio formula ya maisha. Hakuna mtaalamu wa ndoa zaidi ya Bwana Yesu kukaa katikati ya ndao mwenyewe na kujawa na maarifa ya kiuungu ndani yetu. Siku hizi ni za mwisho, wale tulioamua kumtumikia Mungu katika Kristo Yesu tumtumikie kama apendavyo.

Pointi ya nne: Mke ni kiumbe dhaifu hivyo mwanaume anapaswa kuishi naye kwa kwa akili.
Ukisoma 1Petro 3:7 unasema hivi: "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"
Wakati najifunza juu ya mstari huu nilijiuliza maswali mengi sana, nayo ni hya:
1. Biblia imesema mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, je! huu udhaifu umetoka wapi tena?
2. Je! huu udhaifu unaosemwa ni udhaifu upi, wa kiroho au wa kimwili au ni upi? Nilijiuliza sana ikabidi nisome biblia ya Kiingereza na kilugha ili kuweza kuelewa anachotaka Mungu tuelewe. Nikasoma NEW INTERNATIONAL VERSION (NIV) 1Peter 3:7), panasomeka hivi:
"Husbands, in the same way be considerate as you live with your wives, and treat them with respect as the weaker partner and as heirs with you of the gracious gift of life, so that nothing will hinder your prayers.
Bwana Yesu tusaidie hatua kwa hatua jambo hili:
Jambo la kwanza: Biblia inatushauri kukaa na wake zetu kwa akili , ukisoma kwa kingereza anasema "be considerate" ghafla nikaanza kuelewa maana yake nini, considerate imetokana na neno consider, na neno consider   linamaanisha heed, think critically, or pay attention. Nikaanza kupata picha kuwa, considerate humaanisha "be attentive", "be mindful", "be thoughtful", "be careful not to cause harm to others", glory to Jesus!
Hivyo neno ishi na mke wako kwa akili maana yake: 'In whatever you do to your wife, before you do it, be careful not to cause harm to your wife or Be thoughtful when you treat your partner. Maana yake, Jihadhari unapotenda jambo kwa mke wako, lisiwe na madhara kwake kiroho na kimwili.Kwa lugha nyingine, kwa kuwa mke ni dhaifu, ndivyo ameumbwa, chochote unachotaka kutenda kifikiri ikiwa hakina madhara kwake, kwa nini kwa sababu mke anapenda umfanyie mambo anayotaka kwa kumjali, muonyeshe kuwa yeye ni wa thamani kwako. Treat them with respect....let she know that you really value her. 
Hebu tusome haya maaandiko kutoka kitabu cha J.B.PHILLIPS COPYRIGHT. 
Panasomeka hivi " Similary, you husbands should try to understand the wives you live with, honouring them as physically weaker yet equally heirs with you of the grace of eternal life. If you do not do this, you will find it impossible to pray properly"
Hapa anasisitiza hivi: ...try to understand the wives you live with...Maana yake , jitahidi kumuelewa mke wako: Kumuelewaje? Tuchukue mfano: Umetoka kazini ukakuta "mama hayupo, unashangaa anarudi muda ambao hukuzoea, je unachukua maamuzi gani? Kumbuka Biblia inasema, "mke ni dhaifu" nadhani hasira siku zote ni mbaya, lakini ukifuatilia Mungu anachotufundisha hapa utafahamu haraka kuwa " akifika jitahidi kwanza kumpa nafasi ajieleze na unapomjibu Mungu akusaidie usiwe na uchungu naye, maamuzi utakayochukua yasiharibu uhusiano wenu na Mungu, lakini pia yasilete madhara (hurt) kwa mke wako. Kama vile unavyoongea na mtoto mdogo, hivyo hivyo ongea na mke wako. Ukweli ni kwamba tukiwakasirikia hawa wake zetu, tutawaua, kiukweli ni wadhaifu. Tuwatendee kwa upole na kwa utulivu. 
Najua si jambo lepesi, lakini maandiko yanasema " nayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu. Hata wewe unaweza. Mheshimu mke wako, jitahidi kumsikiliza kwa upole na kwa umakini huku ukijitahidi kumuonyesha kuwa unamjali. Akili ya mwanamke inahitaji kusikilizwa na kueleweka. Tujitahidi tusiwe na uchungu nao. Tutaangalia somo hili hatua kwa hatua. Naomba uniombee kwa kadri uwezavyo, Yesu akubariki!    
 

0 maoni:

Chapisha Maoni