Habari za asubuhi rafiki yangu!
Binafsi sijambo, namshukuru Mungu.
Leo nataka tujifunze namna ya kuchukua maamuzi sahihi tunapochukua MIKOPO (LOANS) katika kufanya biashara na matumizi mengine.
Ndugu msomaji wa mtandao huu; nina uhakika unajua kuwa mwanadamu maadamu yu hai hana budi anahitaji kuwa na fedha awe mkubwa au mdogo, awe tajiri au masikini, wote tunahitaji fedha. Huu ndio ukweli wa mambo.
Na katika uhitaji huu, uchumi wa dunia umekuwa ukijifunza na kufanya tafiti nyingi juu ya kuhakikisha kila mtu ili aweze kufanya biashara lazima ahitaji pesa au hela au fedha. Na kwa sababu hiyo, benki nyingi na taasisi mbalimbali duniani zimeanzisha mfumo wa kukopesha na kurudisha faida (riba) kwa aliyekukopesha fedha hizo (loan).
Ndugu rafiki yangu, shida imekuja pale wakopaji wanapojidanganya wakidhani mkopo ni msaada au huduma ya kusaidia wasiojiweza. Namaanisha nini?
Namaanisha kuwa unapokopeshwa fedha ujue aliyekukopa, anahitaji na RIBA katika fedha hiyo, upate hasara au upate faida lazima umrudishie fedha zake pamoja na RIBA. Na si kosa kumpatia RIBA mkopeshaji kwani anafanya biashara.
Riba ni faida utakayomzalishia kwa kipindi maalumu mnachokubaliana kimkataba.
Nachotaka ufahamu ni hiki, aliyekukopa anafanya biashara na wewe, na ukiwa mzalishaji bora unakuwa mwaminifu kwa aliyekukopa.
Zingatia jambo hili: MKOPO ni BIASHARA.
Kwa kuwa siku hizi kumekuwa na ukosefu wa mitaji, taasisi mbalimbali za kifedha zilizo rasmi na zisizo rasmi zimeanzisha huduma za mikopo tena kwa urahisi zaidi, na kadri siku zinavyoendelea, huduma hii ya mikopo inazidi kupamba moto.
Na wahitaji kwa kutokujua hili, wamechangamkia FURSA hizi bila kujiuliza maswali, na hali zao za maisha wengine zimeyumba jumla. Sisemi kwa kukuogopesha, nasema ili ufanye maamuzi mazuri katika masuala ya mikopo.
Natamani nikushauri jambo moja kubwa! Siku zote unapochukua mkopo jiulize maswali yafuatayo:
1.Mkopo huu unatolewa na taasisi ipi?
Si watu wengi sana wanaotafuta mikopo wanajiuliza swali hili, wao wanachotaka ni hela tu, mengine baadaye! Kuwa mwangalifu juu ya hili. Unapotaka kukopa, fuatilia kutaka kujua hiyo taasisi ikoje. Ndiyo maana wengine wameumizwa jumla na wameporomoka kimaisha kwa sababu ya mahali walipochukua mikopo. Nakumbuka mwaka fulani, kuna taasisi walianzisha mfumo fulani, ukitaka mkopo, unatoa hela za kwako kwanza, wao wanakuambia kuwa, inabidi uwekeze kwanza kwao kisha baada ya muda wao watakukopesha fedha za kukutosha. Na kwa kuwa unakuwa na kiu ya fedha, unajikuta umetoa fedha zako. Ndugu msomaji, na mwaka huo watu wengi walitoa fedha zao na mpaka leo, hiyo taasisi ilikopotelea hakujulikani.
Kumbuka kuwa, kuna uhusiano wa karibu kati ya fedha na hali ya kiroho ilikotoka fedha hiyo. Na hiyo roho itafuatilia hizo fedha. Ndiyo maana kuna sehemu ukikopa fedha huzifanyii chochote hata kama umejiandaa kufanya kitu fulani. Ukishazipata tu, akili inafanya kinyume, baada ya fedha kuisha ndipo unashtuka. Ikiwezekana unakopa tena na tena, mwisho wake, unaishia pabaya.
muhimu: Fanya uchunguzi wa kina wa mahali unataka kukopa fedha.
2. Unajua RIBA ya mkopo unaotaka kuchukua?
Ni muhimu na ni lazima uulize wahusika juu ya RIBA zao, na wanakokotoaje hizo riba. Waulize hizo riba ni kwa mwaka au kwa mwezi? Waulize usiwaogope, maana kuna wengine wakifika sehemu hizo utadhani wao ni malaika, waulize vizuri, ukiridhika sawa, usiporidhika achana nao, hiyo ni biashara sio huduma. Kwa mfano, unaweza ukaambiwa riba ni 1.6% , halafu wewe huulizi unajua riba nafuu. Au unafikiri nakutania? Wako watu wengi wamechukua mikopo bila kujua utaratibu wa riba.
muhimu: fahamu kwa undani utaratibu wa riba zao.
3. Je, naruhusiwa kufuta mkopo nje na muda tuliopatana?
Watu wengi hawaulizi swali hili muhimu sana, wao kwao kinachotafutwa ni fedha. Ndugu msomaji, waulize hivi: Naweza kuja kurudisha au kulipa fedha zenu hata kama ni kabala ya muda wa kimkataba? Waulize tena hivi: Mtu anapokuja kufuta mkopo wake, mnatoa riba au hamtoi? Na unapojibiwa waombe vipeperushi au maandiko yanayodhihirisha hayo. Usipende kuambiwaambiwa kwa mdomo tu. Omba kupewa nyaraka.
Lakini pia unaweza ukawauliza: Je, ikatokea nikafa, mkopo wangu utafutwa au waliobaki watawajibika nao? Omba kufafanuliwa vizuri. Kufa kupo maadamu unaishi chini ya jua.
Swali la mwisho, waulize hivi: Ikatokea nimekwama kifedha, naweza kusimamishiwa mkopo kwa muda fulani? Waulize wala usiogope!
4. Jiulize hili swali mwenyewe, "kwa nini nataka kuchukua mkopo?
Ndugu msomaji ni muhimu ujue jibu la swali hili, kwani mkopo ni fedha ya mtu amekupa uizalishe upate faida na mgawane hiyo faida. Ndiyo maana ni muhimu ujue kuwa mkopo ili uweze kumpatia faida yake mkopeshaji na wewe upate faida yako, huna budi kuizalisha. Kuna msingi mmoja wa fedha nao ni huu:Fedha huwakimbia wasiojua kuizalisha.
Usichukue mkopo kufanyia mambo ya ovyo hovyo wakati huna hata kitega uchumi kingine!
Wapo watu wanashangaza mno, wao ilimradi fedha zipo yeye atazichukua tu.
ushauri wangu kwako, usianze kuchukua mkopo mkubwa kwa mara ya kwanza, anza na kidogo ili ujue uwezo wako. Mkopo ni sawa na bunduki ya kuwindia wanyama, ukiitumia vizuri, unampata mnyama huyo, ukiitumia vibaya, unakugharimu wewe mwenyewe.
Nawatakia Jumamosi njema na baraka tele!
Nice ujumbe
JibuFutaUnahitaji mkopo wa 100%? Ninaweza kutumikia mahitaji yako ya kifedha na matatizo mabaya ya kurudi ndiyo sababu tunakufadhili kwa 2% tu. Chochote hali yako, kujitegemea, kustaafu, imepungua rating ya mikopo, tunaweza kusaidia. Flexiblerepayment zaidi ya miaka 1 hadi 30.Chungana nasi kwa: comfortfrankloanfirm@gmail.com
JibuFutaUnatafuta mikopo ya muda mrefu au ya muda mfupi
Jina Kamili: ............................
2 Anwani ya Mawasiliano: .......................
3.Country: .....................
4.Sehemu: ...............
5. Mkopo wa Fedha Inahitajika: ....................
6. Muda wa Mikopo: .....
7. Namba ya simu ya moja kwa moja: .................
Upendo Mengi,
Farajafrankloanfirm@gmail.com
L
Mrs: faraja
Do you need an urgent loan to clear your debts or do you need a equity loan to improve your business? Have you been rejected by banks and other financial agencies? Do you need a loan consolidation or mortgage? Search no more as we are here to make all your financial problems a thing of the past.
JibuFutaThis is an easy loan company. We offer loans to those interested in a reasonable interest rate of 2%. The range ranges from $ 5,000.00 to a maximum of $ 100,000,000.00 dollars.
Our loans are well insured as maximum security is our priority.
Contact us by email: oceanfmortgages@gmail.com
Regards
Max Bent
oceanfmortgages@gmail.com
2% Original Loan and Guarantee
oceanfmortgages@gmail.com
Je, unahitaji mkopo wa haraka? Tunatoa Mikopo ya Kibinafsi? Mikopo ya Biashara? Mikopo ya Nyumbani? Mikopo ya Kilimo? Mikopo ya Elimu? Mikopo ya Ujumuishaji wa Debit? Mikopo ya Lori? Mikopo ya Gari? Mikopo ya Hoteli? Mikopo ya Refinance? na Mikopo zaidi ya Shule? Mikopo ya Kuanzisha? .Tunatoa kwa riba ya 2%! Wasiliana nasi kupitia: richardcosmos5@gmail.com
JibuFuta