Natumaini unaendelea vizuri katika harakati za kupambana na maisha ili uweze kufanikiwa. Ndugu msomaji wa makala zangu, kuna kitu watu wengi wamesahau kukifanya na kinawagharimu mno. Si mara nyingi watu huwa tunajitathmini kwa nini tunakwama kila siku katika kufanikisha ndoto (vision) zetu tulizonazo.
Umewahi kujiuliza kwa nini unakwama kila wakati?
Umewahi kukaa chini angalau muda wa hata nusu saa ili utafakari kwa nini huvuki mahali ulipo kimaisha? Wengi tukikwama huwa tunakimbilia kuwalaumu wengine, hutaona tukijilaumu na kujitathmini sisi wenyewe kwanza; na hii imetufilisi fikra zetu na mitazamo ya kimaisha tuliyo nayo (mindset).
Ulishawahi kujiuliza haya maswali? Nadhani umewahi kujiuliza. Na kama hujajiuliza leo nakushauri kaa chini ujiulize hayo maswali.
Laiti watu wengi tungekuwa na tabia ya kujifunza kutokana na makosa tunayofanya tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
Leo nataka nikupe ushuhuda wa kwangu binafsi ulionisaidia nikaanza kuvuka baadhi ya maeneo, si kwamba nimekwisha kufika, bado napambana kama wewe, ndio maana nakushirikisha ili tupambane wote kuelekea kwenye maendele na mafanikio ya maisha yetu. Unajua dunia hii ina FALSAFA nyingi sana, nyingine zinatusaidia nyingine hazitusaidii. Ni uamuzi wako ufuate "phillosophy" ipi katika maisha yako kwa kuwa maisha ni uchaguzi.
ushuhuda
Mwaka 2013 ni mwaka nimeanza kazi katika taasisi fulani hapa nchini. Nimeanza kazi hiyo pamoja na marafiki zangu kama tano (5) hivi. Nilipoanza kazi nilikuwa na malengo mengi sana na nilijua ndo nimefanikiwa kimaisha jumla.Maisha yaliendelea, na baada ya muda nilianza kupigiwa simu za ndugu na marafiki wakihitaji msaada wa kipesa, na mimi sikuona shaka kuwapa wakati NAJIONA kuwa fedha ninazo japo hazikuwa nyingi. Na ndugu hawa baada ya kuona wakiomba msaada kwangu hawanyimwi waliamua kunitegemea jumla bila ya mimi kujua. Baada ya mwaka mmoja na miezi kadhaa, nilianza kuingia kwenye madeni ya hapa na pale. Kilichonifanya nikajikuta kwenye madeni ni huruma zangu za kuwaokoa ndugu zangu waliokuwa wakihitaji msaada kwangu kifedha.
Maisha yalizidi kuwa magumu hata ikafika mahali nikaaanza kukata tamaa na ndoto zangu. Wakati huo nilikuwa na mchumba au rafiki wa kike niliyekuwa nimemuahidi kumuo siku si nyingi. Ghafla, ugomvi ulianza baina yangu na yeye, hii ilitokana na yeye kuona kuwa nampa ahadi hewa, na hii ni KWA SABABU SIKUMWAMBIA UKWELI KUHUSU hali niliyokuwa nayo.
Siku moja huyo mchumba wangu alinipigia simu usiku. akaniuliza hivi: Faustine! do you really need me to be your wife? Nilimjibu , yes my dear, I do!
Ndipo aliponiuliza hivi, mbona nikikuomba hela hata elfu 10 unaniambia subiri mwisho wa mwezi? Aliongeza tena akasema, kwani kuna shida gani, ni kweli hela huna au una binti mwingine?
Aliendelea kunilaumu sana, na wakati huo nilikuwa napigiwa simu nyumbani kwa kila tatizo lililojitokeza hata kama lilikuwa ndani ya uwezo wao. Madeni yaliendelea kunitesa nikafika mahali hta kukopa siwezi tena. Ndipo nilipoona kuwa maisha yamenishinda, japo kwa nje niliokena ninazo pesa.
Baada ya miaka 2na miezi hivi, nilikuwa hata siwezi kumudu hata kula chakula cha kushiba, nikaona sasa naelekea kufa.
Tarehe 25 ya mwezi Disemba 2015 nikiwa nasherehekea "KRISMASI" lilikuja swali moyoni mwangu, nalo lilikuwa hivi: Nitaishi maisha haya mpaka lini na huku nina AJIRA? Nikajiuliza tena, " kwa nini nisiwashirikishe wazazi wangu, na watu wa karibu kwangu juu ya hali niliyo nayo?
Nikaamua kuwashirikisha wazazi wangu kuhusu madeni na hali niliyonayo. Nilimshirikisha pia mchumba wangu hali niliyokuwa nayo japo kwa aibu.
Wazazi wakaniambia hivi, unajua kwa nini umekwama kimaisha? Nikajibu ndiyo! Baba akaniuliza, ni nini? Nikamwambia "nina wategemezi wengi". Baba akasema "hapana". Tatizo ni wewe mwenyewe!
Alivyosema hiyo sentensi nilifikiria sana kwa nini amesema hivyo.
Ghafla nikagundua jambo lifuatalo ambalo lilibadilisha maisha yangu.
1. Niligundua kuwa nilidhani kwa kuwa ninapata pesa kila mwezi, basi nitafanikiwa.
2. Niligundua kuwa huwa sijifikirii KWANZA kabla ya kuwafikiria wengine.
3. Niligundua kuwa kila hela ndogo ninayoipata ni ya muhimu kwangu.
4. Nilifahamu kuwa, nilitakiwa nijikwamue kwanza mimi ndipo nianze kuwasaidia ndugu zangu.
5. Niligundua kuwa hata fungu la kumi si mtoaji kabisa.
UAMUZI NILIOCHUKUA.
1. Niliamua kuomba toba kwa Mungu juu ya matumizi yangu ya fedha.
2. Nilitengeneza mfumo wa kifedha wa "kuweka akiba kila mwezi " KABLA ya kupanga matumizi ya pesa.
3. Nilianza kuweka vipaumbele katika maisha yangu na kuvitendea kazi.
4. Nilianza kuwekeza pesa nyingine.
5. Nilianza kuishi uhalisia wa maisha yangu.
6.Nilianzisha chanzo kingine cha kipato nje na AJIRA, na hapa ndipo nilipoanza kufurahia maisha kwa kiasi fulani.
Ndugu msomaji, naomba nikushauri mambo yafuatayo:
1. Usiishi jinsi usivyo ili kuwafurahisha wanaokutazama, maana mafanikio yako, yako mikononi mwako.
2.Jizoeze kuweka akiba kwa kila fedha unayopata hata kama ni ndogo.
3 .Usianze kuwabeba wategemezi ulionao wakati bado na wewe umenaswa. Waeleze ukweli kuwa bado kuna mambo unayaweka sawa. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu japo ukweli haupendwi na wengi.
4. Epuka madeni, na kama unayo yalipe kwanza hata kidogo kidogo. Hutaweza kufanikiwa na kuwa huru wakati bado ni mdaiwa. LIPA DENI ULIZO NAZO, waeleze ukweli wanaokudai kuwa utaanza kuwalipa, usiwakimbie kawaeleze ukweli wa maisha yako, nao ni binadamu, watakupa utaratibu wa jinsi utakavyowalipa. DAWA YA DENI NI KULILIPA si zaidi ya hapo.
5. ANZISHA BIASHARA AU CHANZO CHA KIPATO kingine.
6. Amua kuwa utabadilika katika maisha yako, na hapo ndipo utakapoweza kuona mafanikio yako.
Mungu awabariki, wako MASTER WA VIPAUMBELE KWANZA.
0 maoni:
Chapisha Maoni