Ijumaa, 24 Machi 2017

JE, UNAZIJUA KANUNI ZA UFALME WA MUNGU KATIKA KUKUFANIKISHA?

Bwana Yesu asifiwe rafiki! Tumsifu Yesu Kristo!
Ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA nachukua nafasi hii kukupa pole kwa majukumu uliyonayo pamoja na changamoto unazopitia. Hayo hayana budi kuwepo maadamu bado tunaishi katika dunia hii. Lakini nikutie moyo kuwa kila jambo lina majira yake.

           Ndugu msomaji, uwe mkristo usiwe mkristo sisi wote Mungu anapenda kutufanikisha. Yesu hakuwafia wakristo bali alikufa kwa ajili ya ulimwengu na wewe ukiwemo. Kuna maswali ambayo watu tumekuwa tukijiuliza mara kwa mara bila majibu. Na kwa kuwa dunia hii ina wasomi wengi tumefika mahali tumemwekea Mungu wetu mipaka. Hivyo tumeamini wapo watu tukiwaeleza matatizo tuliyo nayo yataisha, lakini tunakuja kukumbuka kuwa bado yanajirudia kwa kuwa bado hatujapata ufumbuzi wake halisi. 
 Swali ambalo limekuwa likinisumbua kwa miaka mingi ni hili: Kwa nini watu wanaomwamini Mungu hawafanikiwi kiuchumi wakati Bwana Yesu ameahidi kutufanikisha? Je, neno la Biblia ni neno la Mungu kweli au ni kitabu tu cha kihistoria? Kama Mungu anatupenda si atupatie mafanikio sisi tulio watoto wake?
       Siku moja nilikuwa natafakari juu ya jambo hili, wakati natafakari nikawa nasoma huu mstari katika Biblia " Mathayo 6:33, Bali utafuteni kwanza Ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa". 
Niliendelea kutafakari huu mstari kwa muda mrefu sana, baada ya muda nikaona kitu ambacho kilibadilisha maisha yangu kiroho na kiuchumi hatua kwa hatua. Andiko hili linasema hivi, Tafuta kwanza Ufalme wa Mungu, Biblia haisemi, Omba kwanza ufalme wa Mungu Uje, no! no! no! Biblia inasema tafuta. Tafuta..haisemi, Omba Ufalme wa Mungu uje, hapana..
Wakati naendelea kuwaza kwa kina juu ya mstari huu, nikasikia wazo moyoni mwangu..watu wengi wanafikiri kutafuta ufalme wa Mungu ni kuokoka au kuzaliwa upya mara ya pili kwa Roho Mtakatifu, lakini si hivyo. Kutafuta Ufalme ni kusoma neno la Mungu kwa msaada wa Roho wa Mungu na kwa maombi, huku ukimuuliza Mungu unachotaka. Wakati naendelea kutafakari hili wazo lililokuwa ndani yangu, nikakumbuka ule mstari wa Hosea 4:6 usemao, "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa..
Ndugu msomaji, fahamu jambo hili katika maisha yako, katika nyakati hizi za mwisho, kila mtu anataka kufanikiwa hasa kiuchumi, na ni jambo zuri, lakini tamaa hii haitufikishi popote. Tunapata pesa nyingi, lakini zinapotea bila maelezo, tunaanza upya. Tunajitahidi hata kufuata ushauri tunaopewa na wataalamu wa masuala ya kifedha lakini bado tunakwama. Sikia na uelewe, kama unataka kuona Mungu akikufanikisha, huna budi kujua na kufuata misingi/kanuni zilizoko katika Ufalme wa Mungu katika neno lake. Kuwa mtoto wa Mungu tu haitoshi kufanikiwa kiuchumi mpaka utakapojua misingi iliyo katika neno lake na kuitenda, haleluya!
Jambo la kukumbuka ni hili, Unataka kufanikiwa ili ufanye nini na hayo mafanikio?
Kwa sababu Mungu akikufanikisha anataka aliweke imara AGANO LAKE. Ikiwa kusudi lako la kufanikiwa si kuimarisha Agano la Mungu, sahau mafanikio Kimungu ("Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye atupaye nguvu za kupata Utajiri; ILI ALIFANYE IMARA AGANO LAKE alilowapa baba zako, kama hivi leo" (Kumbukumbu la Torati 8:18).
Ukisoma vizuri maandiko matakatifu kwa msaada wa Roho Mtakatifu, utagundua kuwa bado kuna mambo mengi hatujayajua na kwa sababu hiyo, tunapoyatenda hatupati tunachotaka kwa kuwa hatuyaelewi vizuri tunayatumia isivyo (misapplication of holy scriptures). Soma pia nafasi ya mwanamke kibiblia

Ndugu msomaji naomba Mungu akupe ufahamu na afungue macho yako ya ndani uone kile Mungu anachotaka uone katika neno lake. Pia nikushauri jambo hili, jizoeze kujiombea kwa Mungu ili akupe kulijua neno lake swasawa na jinsi anavyotaka ujue, na ukishajua tenda kile neno linataka. Hili somo litakuwa na mwendelezo kwani ni somo refu sana.
Na usisahau kuniombea ikikupendeza kwani hatuwezi kuandika haya mambo bila msaada wa Mungu. 
Karibu tufuatane pamoja katika utangulizi huu!
Ukurasa wa 1.
  • Ni kusudi la Mungu kutufanikisha. 
 Ukisoma Waefeso 5:17, Utagundua jambo lifuatalo;
Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Ukirudi nyuma mstari wa 16, utagundua kwa nini amesema 'kwa sababu hiyo'..Sababu ipi?
Verse 16. Zamani hizi ni za uovu, na ule wa 15, unasema, tuenende kama watu wenye hekima, hekima hii inapatikana katika neno lake.
Maandiko yanasema, tusiwe wajinga, kwa hiyo tujitahidi kuyajua mapenzi ya Bwana (will of the Lord). Hivyo amini moyoni mwako kuwa Mungu anao mpango wa kukufanikisha.
Ukisoma Waefeso 5:14, maandiko yanatuambia, Amka wewe usinziae....na Kristo atakuangaza.

Jambo la 2: Tafuta Ufalme wa Mungu na haki yake.
Ukisoma (Mathayo 6:33), Biblia inasema, Tafutaeni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake, na hayo yote, mtazidishiwa. Tunapaswa kutafuta kujua makusudi ya Kimbingu juu ya hicho tunachoomba tupewe. Tunatafutaje? (a) Kwa njia ya neno lake
(b) Kwa kumuomba Mungu huku tukimuuliza. Maana ukisoma Isaya 45:11, Niulize.....
Laiti watu wa Mungu tungefuata kile neno linachotushauri, nina uhakika tungetambua ukuu wa Mungu..Je, tunayajua mapenzi ya Mungu katika shughuli zetu na biashara zetu? Je, huwa tunautanguliza ufalme wa Mungu

Jambo la 3: Amini moyoni mwako kuwa Mungu anafurahia mafanikio yetu (watoto wake).
Soma Zaburi 35;27; Mathayo 7:11,....Biblia inasema, japokuwa sisi tulio waovu tunajua kuwapa watoto wetu vipawa vyema, je, Yeye Mungu asiye muovu si zaidi sana anatamani kutufanikisha zaidi? Oo..haleluya!
Sikia mtu wa Mungu, acha kumlaumu Mungu wetu, eti anatupa umaskini ili tunamwabudu, si kweli na haipo katika neno lake, Mungu hatuonyi kwa kutumia umaskini bali kwa kutumia neno lake...

Jambo la 4: Mpango wa Mungu kwetu ni kuwa na vingi tele. Soma Warumi 12:2, Yohana 10:10.
Mungu anavyo vitu vingi na utajiri mwingi na anatamani atupe hivyo vitu..Kumbuka kuwa Mungu anavyo vitu vyote na anatamani atufanikishe kwa kadri ya alivyo navyo...
Hagai 2:8, Mwanzo 15:5. 

Jambo la 5: Jua uhusiano uliopo kati ya Mungu, Neno la Mungu, na wewe (Mimi).
God, His word and You.

 

0 maoni:

Chapisha Maoni