Ijumaa, 3 Februari 2017
Habari za asubuhi ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA!
Mimi nami namshukuru Mungu wa mbingu na nchi.
Asubuhi hii naomba nikuulize hili swali moja tu: "Kwa nini umekwama jumla
kimafanikio"? Yapo mambo mengi unayoweza kuzungumzia kama vizuizi vya
kufikia mafanikio yako. Na mimi nakubaliana na wewe kuwa vikwazo ulivyo
navyo ni sahihi. Lakini naomba tutajidili kikwazo kimoja kikubwa ambacho ni
uvivu wa kuweka akiba kutoka kwenye pato lako.
Ndugu msomaji huwa unakumbuka kuweka AKIBA kila upatapo pato lako?
Kama unaweka akiba, hongera sana; na kama huweki akiba , amka sasa uanze
kuweka akiba (SAVINGS). Akili isiyojizoesha kuweka akiba inajiandaa kuwa
mtumwa kifedha. Huwezi kukwepa huu ndo uhalisia wenyewe. Nakuomba jitahidi
uwe na AKIBA ya kutosha, hakikisha kila wakati unapopata fedha, anza na akiba.
Save as much as you can for your future. Nikutakie asubuhi njema!
0 maoni:
Chapisha Maoni