Jumanne, 31 Januari 2017

JE, HUWA UNAJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA UNAYOFANYA JUU YA FEDHA?

Habari za kuamka ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA! Mimi nimeamka salama namshukuru MUNGU wa Ibrahimu, na Isaka na Yakobo. 
     Napenda asubuhii tutafakari jambo moja muhimu ambalo kwa sehemu kubwa limetukwamisha tulio wengi hasa katika masuala ya fedha.

Je, huwa unajifunza kutokana na makosa unayofanya juu ya matumizi ya fedha?
Mara nyingi utakuta wengi wengi wanapoona mipango yao ya kimafanikio haipigi hatua hasa katika masuala ya fedha utashangaa kuona anayeanza kulaumiwa ni aidha Serikali, watu wengine au Shetani. 
Ushuhuda: Tangu mwaka 2011 na 2012 nimewahi kupata pesa za kutosha katika maisha yangu. Lakini kilichoniumiza zaidi ni kuona sisogei nipo palepale siku zote. Nilijaribu kuwalaumu watu mbalimbali lakini haikutosha na haikunisaidia. Siku moja usiku nikiwa nimelala lilikuja swali akilini mwangu, nalo lilikuwa hivi:
Kwa nini kila siku nina maisha magumu wakati napata pesa nyingi kiasi hiki na wakati sina matumizi mabaya ya fedha? Tatizo liko kwangu au kuna watu wanaonifanyia ubaya ili nitumie fedha isivyostahili? Je, ninawategemezi wengi ? Je, ninaishi kwa kujionyesha kwa watu kama vile nina pesa nyingi? Baada ya kujiuliza maswali mengi kama hayo hapo juu, nilisukumwa kuomba TOBA baada ya kugundua mimi ndiyo chanzo cha tatizo hilo. Nilitambua kuwa, "nilikuwa naishi kwa kujionyesha kuwa nina pesa na kwa sababu hiyo yeyote aliyeniomba pesa nilikuwa nampa. Nikawa najikuta mwisho wa siku sina pesa. Nilipoanza usomaji wa mwandishi mmoja wa kitabu aitwaye DAVE RAMSEY nilipata wazo moja ambalo lilinivusha kwa kiwango kikubwa. DAVE RAMSEY anasema hivi:" Live as a poor in all circumstances while you are SAVING and INVESTING the money you earn". Huyu ndugu anasema hivi:
Ishi kama maskini wakati uo huo ukiwa unaweka AKIBA & na UNAWEKEZA pesa unazopata. Ushauri wangu: Jifunze kutokana naamakosa unayofanya upate kijifunza zaidi kutokana na makosa hayo. 
Usikate tamaa unapogundua umefanya makosa katika eneo lolote, dawa ni kujua kwa nini unakosea na kujirekebisha. Nikutakie siku ya fanaka na Mungu awe nawe katika shughuli zako zote, wako katika VIPAUMBELE KWANZA blog.

0 maoni:

Chapisha Maoni