Leo napenda nikushirikishe jambo hili muhimu moja tu unalopaswa kulikumbuka kila siku. Kabla ya kukueleza hili jambo moja; hebu tujiulize haya maswali. Lengo la kujiuliza haya maswali ni kutokana na mitazamo ya watu juu ya mafanikio yao kiuchumi.
Watu wamekata tamaa utadhani maisha ndo basi. Wengine wakikumbuka wingi wa pesa zilizopita mikononi mwao wanaishiwa nguvu kabisa. Ukweli ni kwamba mafanikio yako hayatokani na pesa unazotengeneza/unazopata bali maamuzi unayochukua juu ya hizo fedha bila kujali kiwango cha pesa ulichonacho. Ndugu msomaji, acha kukata tamaa, acha kujilaumu, acha kunung'unika, cha msingi fanya jambo moja kwanza tu, hayo mengine hayana budi kuja.
Muhimu ni kujizoeza kuwa na subira, maana mafanikio ya kweli yanahitaji muda mrefu hasa kwa wale ambao ndo wanavuta kasia. Usiwaone matajiri wa leo hawakuanza leo bali wanamuda mrefu.
Yapo mambo mengi ya kujifunza sana juu ya mafanikio na uchumi. Kadri tutakavyopata nafasi tutazidi kujadili mambo ya kuzingatia ili tuweze kuvuka mahali tulipokwama.Soma pia
TRIANGLE FINANCIAL PRINCIPLES
Kabla ya jambo hilo tujiulize maswali yafuatayo:
1. Unapata fedha kiasi gani kwa siku?
2. Una wategemezi wangapi wanaokutegemea?
3. Ni vizuizi gani vilivyokuzuia usifikie malengo yako?
4. Ni lini umejipanga kutoka kwenye umaskini?
5. Ni mkakati gani uliouandaa kukutoa hapo ulipo katika mafanikio yako ya kifedha?
Ndugu rafiki unayesoma somo hili, hapo juu umejiuliza hayo maswali 5, mengine utajibu wewe mwenyewe, mimi nitajibu hili la 4 na 5 tu.
Ukiona mtu yeyote asiyejiuliza maswali katika yanayomhusu si rahisi kutoka mahali alipo.
Swali la 4 linasumbua sana watu waliowengi wanaweka malengo yao bila kuhusianisha na muda, na kwa sababu hiyo wanakosa uvumilivu na hamasa ya kusubiria hicho wanachokitaka. Naomba nikushauri kuwa kila lengo unaloweka liwekee muda wake.
Katika swali la 5, tumejiuliza kuwa ni lazima tuwe na mkakati thabiti wa kutusaidia kufikia malengo yetu. Kila mmoja wetu anapaswa kuwa na njia au utaratibu wa uhakika sio wa kusadikika. Leo nataka nikukumbushe njia au utaratibu huu mmoja tu.
Jiwekee utaratibu wa kuwekeza fedha zako kila unapopata pesa. Ziwe nyingi au kidogo. Kwa mfano, fungua account bank inayotoa riba na kila mwisho wa mwezi weka (mfano 50,000 tshs) ila usiombe ATM CARD. Ngoja nirudie tena, tafuta taasisi inayoaminika na inayotoa riba nzuri, fungua akaunti na anza kuweka fedha kidogo kidogo kila mwezi, na fanya hivyo kwa muda mrefu kama miaka 5 hadi 10. Nakueleza ukweli ukiweza hili umeweza kufanikiwa. Jambo hili ukilifanya huna budi kutoka ulipokwamia na utashangaa hata wewe mwenyewe. Zipo taasisi kama UTT Amis au EXIM BANK wanazo hizi huduma. Ila ningekushauri uanze kuwekeza UTT Amis kwani wana riba nzuri. Sikulazimishi ila hapo ndipo na mimi ninapowekeza!
Uvumilivu ni muhimu lakini wazungu husema, "Investing is the magic financial compounding" wakimaanisha kuwa, uwekezaji ni mfumo unaokulipa kwa kushangaza mno.
Nikutakie utekelezaji mwema, wako kocha na mjasiriamali Faustin Mahende, nipigie simu kwa namba zifuatazo:
+255 765 977 026
facebook: Mlishi Mahende
Twitter: Mlishifaustin@Mlishifaustin.
0 maoni:
Chapisha Maoni