Ijumaa, 27 Januari 2017

KIZUIZI KIKUBWA CHA MAFANIKIO YAKO HIKI HAPA

             
 Habari za kuamka ndugu zangu! Mimi nimeamka salama namshukuru Mungu kwa kutupa 
kibali tena siku ya leo..Haijalishi umeamkaje kiafya, kiuchumi n.k. jipe moyo mkuu hayo ni mapito tu..Kila jambo lina mwisho wake.
 Asubuhi hii naomba tutafakari kwa pamoja huu ujumbe. Unakijua kizuizi (obstacle) kikubwa
katika kufikia mafanikio yako kiuchumi? Vipo vizuizi vingi sana, na kila mmoja akipewa nafasi ya kujitetea nina uhakika tutapata vizuizi vingi sana. Lakini nina uhakika kama wote tutatafakari ipasavyo tutakubaliana..
        
         Kizuizi hiki ni MAAMUZI tunayofanya tupatapo pesa katika kutekeleza VIPAUMBELE VYETU, ziwe nyingi au chache..
Mwaka 2015 mimi na rafiki yangu mmoja hivi, tulipata fursa ya kikazi kwenda mkoa fulani,
tulifanya yaliyotupeleka huko kwa muda wa wiki mbili hivi. Baada ya trip hiyo tulilipwa kiasi cha Tsh.900, 000/= kila mmoja. Baada tu ya malipo hayo kila mmoja wetu alifanya MAAMUZI mara moja juu ya FEDHA hizo tulizopata. Huyu rafiki yangu alinunua zawadi nyingi sana akawapelekea wazazi na ndugu zake wengine. Baada ya muda wa miezi 2 akaniambia "my friend pesa ni mavi ya shetani". Nikamuuliza kwa nini? Akasema "huwezi amini ile hela yote imeisha na sijaifaidi". Nilimjibu hivi: Acha kulalamika hayo ndiyo MAAMUZI uliyo fanya mwenyewe, lazima uvune ulichokipanda. Naomba nikueleze jambo hili, siku zote upatapo pesa iwe ndogo au kubwa , jizoeze kutuli kwanza moyoni mwako, kisha fanya maamuzi stahili ambayo hayatakuacha na masononeko. Kumbuka hili kila siku
KILA PESA UNAYOIPATA INAWEZA KUKUTAJIRISHA AU KUKUFANYA MASIKINI ikiwa utafanya maamuzi mazuri au mabaya. 
            Rafiki yako katika safari hii ya mafanikio. Nakutakia shughuli njema!


      

0 maoni:

Chapisha Maoni