Alhamisi, 26 Januari 2017

UMEKWAMISHWA NA NINI RAFIKI?





Ni kweli kila mmoja wetu anaweza kukwama kimaisha kutokana na sababu mbalimbali baadhi zikiwa na ukweli na nyingine zikiwa hazina ukweli.
Swali linakuja: Je!kwa kuwa kuna sababu za kweli tuendelee kukwama
kiuchumi? Nadhani jibu ni hapana. Au nimekosea? Je! akija tajiri akakuuliza swali hili: Niambie kinachokukwamisha kiuchumi nikusaidie. Ungemwambia nikitu gani kikubwa kinachokufanya usipige hatua? Fanya homework hii...Ukipata jibu liandike. Nikirejea hewani nitajadili na wewe jambo hili..

Maoni 3 :

  1. Tutajifunza zaidi juu ya kutathmini fikra zetu ili ziweze kutusaidia kufanikiwa kimaisha. Lakini pia tutajifunza jinsi ya kuondokana na madeni sugu yanayofanya watu wawe watumwa.

    JibuFuta
  2. Karibu rafiki yangu tukishirikiana twaweza...namba zangu za simu ni 0765977026

    JibuFuta
  3. Habari za kuamka rafiki yangu? Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama. Ashukuriwe Mungu aliyetuamsha salama. Asubuhi hii nataka nizungumzie mambo mawili tu:

    MOJA: Kwa nini mara nyingi watu hulalamika kila wakati wakisema maisha ni magumu? Huu ugumu wa maisha utaisha lini?

    PILI: Kwa nini katika mazingira hayohayo mwingine anafanikiwa kimaisha na mwingine anakwama?

    Napenda nikwambie hivi, kamwe hutakuja utoke mahali ulipokwama mpaka uache kwanza kulalamika lakini pia lazima ukiendelea kulalamika macho yako hayaoni FURSA zilizopo kwa sababu unapolalamika, maana yake huoni njia nyingine ya kutatua matatizo yanayokukabili. Watu wa namna hii changamoto kwao wanaiita "maisha ni magumu" (hard life). Hivi ikatokea umeamka ukajikuta uko katikati ya msitu, utaanza kulalamika au utafanyaje? Jambo lolote unalolilamikia uwe na uhakika huwezi kulifanya. Kumbuka jambo hili kila uamkapo, "kulalamika au kunung'unika kunaua mfumo wako wa kufikiri (mindset).

    JibuFuta