Karibu tena ndugu msomaji wa VIPAUMBELE KWANZA!
Najua umechoka na shughuli za hapa na pale za siku ya leo. Pole sana rafiki. Katika usiku huu naomba nikufikirishe jambo moja tu la muhimu kwetu. Ukitazama muda kimwaka (kwa kuangalia urefu wa mwaka utadhani hutazeeka. Hata mimi nilikuwa nawaza sana juu ya hili, lakini ukitizama muda kidakika au kimasaa, utagundua tuna siku chache sana. Kama mwaka una siku 365, bado ni chache sana. Hivyo ni bora tukaanza kujiandaa tutakavyoishi kifedha. Kumbuka kuwa utakapokuwa mzee hutakuwa na nguvu za kufanya kazi tena kama mwanzo, lakini pia usiweke sana tumaini kwa watoto wako hata kama umewasomesha, kwani wanaweza kukukwamisha. Hivyo ili kujiandaa ipasavyo nakushauri ufanye mambo makubwa mawil. Lakini usisahau, tunazungumzia kifedha.
Moja, anza kuwekeza fedha zako kwa taasisi zinazotoa riba nzuri kwa muda mrefu kama miaka 5 au zaidi. Kila fedha unayopata usisahau kutenga sehemu ya kuwekeza.
Pili, hakikisha una kitega uchumi kizuri kitakachokuwa kinakuzalishia fedha wakati wewe huna nguvu tena.
Nikutakie usiku mwema rafiki yangu, na Mungu akulinde.
0 maoni:
Chapisha Maoni